Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe akiwa amembatana na Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt Leonard Akwilapo pamoja,na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Stanslaus Nyongo amefanya mkutano na wananchi wa kata ya zingiziwa eneo la Chanika Wilayani Ilala kwa lengo la kushughulikia mgogoro wa siku nyingi wa mipaka kwenye eneo hilo.
Mkutano huo ni kufuatia utekelezaji wa maagizo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Deogratias Ndejembi alipofanya ziara ya kutembelea dampo la Pugu Jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka viongozi hao kushughulikia mgogoro wa mipaka ya kiutawala kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kwenye kata ya Zingiziwa pamoja na mgogoro wa mpaka kati ya wananchi wa kata hiyo na hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi.
Akizungumza mara baada ya kusikiliza hoja na malalamiko ya wananchi Profesa Shemdoe ametoa muda wa wiki mbili kuanzia leo Sept 23,2026 kwa wataalamu kutoka TAMISEEMI,Wizara ya ardhi pamoja na wataalamu kutoka wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kufuatilia vipimo vya mipaka ili kupata ufumbuzi na watafika tena katika eneo hilo baada ya wiki mbili huku akiwaahidi kumaliza migogoro hiyo ndani ya muda wa mwezi mmoja hadi miwili
Kwa upande wa Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo amesisitiza kuwa wizara yake inaitambua migogoro hiyo hivyo wanakwenda kushughulikia huku Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Hamad Chande akisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita ni sikivu hivyo suluhu ya migogoro hiyo itapatikana mapema iwezekanavyo.
Sanjari na hilo Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewahakikishia wananchi wa maeneo hayo kuwa katika kipindi chote ambacho migogoro hiyo inashughulikiwa hakutakia na vitendo vya uvunjifu wa amani huku akiwataka wananchi kuwa wastahamilivu
Awali wananchi wa eneo hilo walipata wasaa wa kueleza namna migogoro hiyo imekuwa ni changamoto kwenye maisha yao huku Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo akiahidi kuendelea kushuhjulikia migogoro ya ardhi ili kumaliza maumivu waliyonayo wananchi kwenye ardhi





