Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

Mwenge wazindua madarasa Kagongwa – HabariLeo

By admin
August 21, 2026 2 Min Read
Comments Off on Mwenge wazindua madarasa Kagongwa – HabariLeo

SHINYANGA: Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, ameweka jiwe la msingi la jengo la vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kagongwa iliyopo Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Ujenzi wa jengo hilo ulianza kwa nguvu za wananchi waliotoa mchango wa shilingi milioni saba, huku ukamilishaji wake ukifadhiliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kupitia mapato ya ndani kwa kiasi cha Sh milioni 63.

Mwang’onda alisema hayo leo baada ya Mwenge wa Uhuru kupokelewa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kagongwa ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, alipokea mwenge huo.

Amesema amefurahishwa na hatua ya wananchi kushirikishwa katika ujenzi huo na amekubali kuweka jiwe la msingi kwa kuwa mradi huo umefikia hatua nzuri ya ukamilishaji. Aidha, aliwataka wazazi kusimamia maendeleo ya watoto wao na kuhakikisha wanapata elimu bora ili waweze kufaulu katika masomo yao.

Mwang’onda pia aliikabidhi shule hiyo cheti kwa ajili ya Klabu ya Wapinga Rushwa yenye wanafunzi 60, iliyoanzishwa mwaka 2023. Amesema klabu hiyo inaendelea kutoa elimu na kushiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa, jambo ambalo ni muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa salama.

“Nimezindua pia upandaji wa miti katika shule hiyo. Mazingira yanapaswa kutunzwa na kusimamiwa vizuri, na kila mwanafunzi anatakiwa awe na mti wake wa kuutunza. Hii itasaidia kuboresha mazingira ya kujisomea,” amesema Mwang’onda.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, amesema mwenge huo utakimbizwa katika halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na Kahama.

Amesema mwenge huo utapita kwenye miradi 21 yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.4 na utakimbizwa umbali wa kilomita 361.4.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

MAKAME AWAKALIA KOONI MA-DC, UTITIRI WA VITUO VYA UKAGUZI

Next

Bundesliga Kufunguliwa Rasmi Agosti 28, Bayern Munich Kuanza Kazi Nyumbani

Recent Posts

  • Mwang’oda aagiza usimamizi miradi ya CSR – HabariLeo
  • Kagera yapokea vifaa kilimo cha umwagiliaji – HabariLeo
  • Mikakati yasukwa kuvutia wawekezaji wakubwa Ulaya – HabariLeo
  • Majirani jengeni utamaduni wa kutambuana – HabariLeo
  • Bahasha yenye jina la Makamu wa Rais Mteule yatua bungeni – HabariLeo

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme