Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Sample Page
  • Home
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

PROF. MKUMBO: HALMASHAURI ZIBUNI SHUGHULI MPYA ZA KIUCHUMI, SI TOZO MPYA.

By admin
August 19, 2026 2 Min Read
Comments Off on PROF. MKUMBO: HALMASHAURI ZIBUNI SHUGHULI MPYA ZA KIUCHUMI, SI TOZO MPYA.

Na Moses Ng’wat, Songwe.

HALMASHAURI nchini zimetakiwa kuachana na utaratibu wa kuongeza tozo katika vyanzo vilevile vya mapato na badala yake kubuni shughuli mpya za kiuchumi na uwekezaji zitakazoongeza mapato bila kuwaongezea mzigo wananchi.

Wito huo umetolewa Agosti 19, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, wakati akifungua Songwe Dira Forum mkoani Songwe, mkutano unaolenga kuoanisha sekta ya umma na binafsi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Prof. Mkumbo amesema Halmashauri zinapaswa kubadili fikra na kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kuanzisha shughuli mpya za uzalishaji, biashara na uwekezaji badala ya kutegemea kuongeza tozo kwa wananchi na wafanyabiashara wale wale kila zinapohitaji kuongeza mapato.

“Haiwezekani ukawa unakamua tu hadi Ng’ombe anakonda,” alisema Prof. Mkumbo, akisisitiza umuhimu wa Halmashauri kuwa wabunifu katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato.

Amesema kila Halmashauri inapaswa kujitathmini na kubaini angalau fursa tano kubwa za kiuchumi zilizopo katika eneo lake, kisha kuzifanyia kazi ili ziweze kuzalisha ajira, uwekezaji na mapato kwa mamlaka hizo na wananchi.

Amesema utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 haupaswi kubaki katika mipango ya Serikali Kuu pekee, bali unahitaji mikoa na Halmashauri kuweka mikakati ya kutumia rasilimali na fursa zao kuibua shughuli mpya za kiuchumi zitakazochochea maendeleo.

Kwa mujibu wa Prof. Mkumbo, ubunifu huo utasaidia Halmashauri kuwa na vyanzo endelevu vya mapato, kuongeza ajira na uwekezaji, huku wananchi wakinufaika na fursa mpya badala ya kuendelea kubebeshwa tozo katika vyanzo vilevile.

Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inataka kubadili mtazamo wa maendeleo kwa kuifanya Serikali na mamlaka zake za maeneo zisitazame maeneo yao kama vitengo vya kiutawala pekee, bali pia kuwa vitovu vya shughuli za kiuchumi na uwekezaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Makame, amesema maendeleo yanayotekelezwa mkoani humo yanalenga kuweka msingi wa mkoa huo katika kutimiza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Maendeleo tunayoyafanya si kwa ajili ya leo pekee, bali tunajenga msingi wa Songwe tunayoitaka ndani ya Dira ya Maendeleo 2050,” alisema RC Makame.

Mwisho.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Sh4.9 bilioni zalipwa kwa waliopisha mradi wa maji Chamwino Ikulu

Next

Binti auawa kwa madai ya kupigwa na baba yake mdogo, kisa sherehe ya tohara

Recent Posts

  • Mkakati wa kukabili uhaba wa maji na njaa, kuongeza tija ya kilimo
  • Mambo wachumba wanayosahau kabla ya ndoa, madaktari waonya
  • Kesi ya ugaidi mhadhiri UDOM, vigogo CWT zatupwa wiki ijayo
  • DC HAI AENDELEA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI, ATATUA MIGOGORO YA ARDHI
  • Wamiliki miundombinu muhimu ya Tehama watakiwa kuisajili

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme