Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Sample Page
  • Home
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

Sh4.9 bilioni zalipwa kwa waliopisha mradi wa maji Chamwino Ikulu

By admin
August 19, 2026 2 Min Read
Comments Off on Sh4.9 bilioni zalipwa kwa waliopisha mradi wa maji Chamwino Ikulu

Dodoma. Mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka minne kati ya wananchi 880 waliokuwa wakidai fidia ya kupisha kwenye chanzo cha maji, Chamwino umefikia mwisho kwa Serikali kulipa Sh4.9 bilioni.

Katika kipindi hicho, kulikuwa na mvutano kati ya Serikali na wananchi wa vitongoji vya Mpera na Sokoine wilayani Chamwino waliopisha hifadhi ya chanzo cha maji cha Bonde la Chamwino.

Akizungumza jana Agosti 18,2026 Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew, alisema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kutambua umuhimu wa chanzo hicho katika kukidhi mahitaji ya maji yanayoongezeka katika Jiji la Dodoma.



Kundo alisema Serikali ilipohamia Dodoma mwaka 2017, mahitaji ya maji yameongezeka kwa kasi kutoka lita 45 milioni kwa siku, hadi lita 159 milioni, wakati uzalishaji wa sasa ukiwa takribani lita 88 milioni.

Alisema hali hiyo inaifanya hifadhi ya vyanzo vya maji kuwa jambo la msingi katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa uhakika, hususani wakati mahitaji yakiendelea kuongezeka kutokana na ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi.

“Eneo la Bonde la Chamwino lilitengwa tangu kipindi cha Serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, lakini mchakato wa kuwalipa wananchi walioathiriwa umefanikishwa, sasa tunaomba ushirikiano kati ya wananchi na watu wa bonde ili kulinda vyanzo hivi,” alisema Kundo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri, alisema eneo hilo lilitengwa awali likiwa na ukubwa wa takribani ekari 740, ambapo kati ya mwaka 1970 na 1980 Serikali ilichimba mabwawa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima na wafugaji.

Mwajuma alisema baada ya Dodoma kutangazwa kuwa makao makuu ya nchi mwaka 1973, mahitaji ya maji yaliongezeka na eneo la hifadhi likapanuliwa hadi kufikia takribani ekari 2,100, hatua iliyohusisha maeneo yaliyokuwa yakimilikiwa na wananchi na baadaye kusababisha migogoro ya ardhi.

Mmoja wa wanufaika katika fidia hiyo, Elisa Nyembela alisema malalamiko ya fidia katika eneo hilo yalianza tangu 1996 Serikali ilipoongeza ukubwa wa eneo na kuchukua mashamba ya watu nje ya mipaka ya awali.

Nyembela alisema katika kipindi chote hicho wameishi kwa kutegana kati ya wananchi na viongozi ambapo kila upande ulisimamia masilahi yake.

“Leo hii tunaona nuru, danganya toto ilishakuwa ya muda mrefu sana kila wakati kukawa na kauli za malipo ya mwezi ujao, ulifika wakati hatukuamini kitu chochote kilichotokana na kauli za viongozi,” alisema Nyembela.

Malipo ya waliopitiwa na mradi  yalianza jana ambapo wananchi wa vijiji vya Chamwino na Buigiri walipokea hundi za malipo yanayofanyika katika ofisi ya serikali ya Kijiji cha Chamwino Ikulu.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Serikali yasitisha leseni ya MwanaHALISI, TEF yapinga

Recent Posts

  • Sh4.9 bilioni zalipwa kwa waliopisha mradi wa maji Chamwino Ikulu
  • Serikali yasitisha leseni ya MwanaHALISI, TEF yapinga
  • Kilomita sita kufuata matibabu zawasukuma Kola kujenga zahanati 
  • FIFA IMEJIHARIBIA YENYEWE KWA MPANGO WA KOMBE LA DUNIA – MKUU WA LIGI KUU YA UINGEREZA
  • SERIKALI YATOA MIEZI SITA KUSAJILI MIUNDOMBINU MUHIMU YA TEHAMA

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme