Cardi B Avamia Jalada la Vogue Arabia, Aonyesha Mvuto wa Kiarabu

Msanii wa kimataifa kutoka Marekani, Cardi B, amepewa nafasi ya kipekee kwenye jalada la toleo la Septemba 2026 la Vogue Arabia, katika picha iliyozua gumzo kutokana na mtindo wake wa kipekee wenye mguso wa utamaduni wa Kiarabu.

Jalada hilo, lililotolewa Agosti 27, 2026, linamuonyesha Cardi B akiwa amevalia vazi la kifahari lenye mchanganyiko wa rangi nyeusi na kijani, huku akiwa ameshikilia tufaha.

Kinachovutia zaidi ni ujumbe ulioandikwa kwenye jalada hilo, “Assalamu Alaikum, Cardi B”, ambao umeongeza mvuto wa picha hiyo na kuonyesha namna msanii huyo anavyoendelea kuhusishwa na utamaduni wa eneo la Arabia.

Katika toleo hilo, Vogue Arabia imemzungumzia Cardi B kwa upana, ikigusa safari yake ya muziki, mitindo, umaarufu pamoja na maisha yake nje ya jukwaa akiwa mama.

Jarida hilo limemuelezea kama msanii mwenye uwezo mkubwa wa kubadilika kimtindo bila kupoteza utambulisho wake.

Cardi B naye ameonyesha furaha yake kupitia mitandao ya kijamii, ambapo amewashukuru Vogue Arabia pamoja na mpiga picha na mkurugenzi wa ubunifu Szilveszter Makó kwa kazi hiyo.

Mwonekano wake umeendelea kuzungumziwa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimpongeza kwa kuonekana tofauti na vile walivyozoea kumuona kwenye matukio mbalimbali.

Cardi B si mgeni katika eneo la Mashariki ya Kati. Amewahi kutembelea Saudi Arabia na kutumbuiza katika tamasha la MDLBEAST Soundstorm jijini Riyadh.

Safari hiyo pia ilimpa nafasi ya kueleza hisia zake kuhusu watu na utamaduni wa Saudi Arabia, huku akionyesha kuvutiwa na baadhi ya vipengele vya utamaduni huo.

Kwa jalada hili la Vogue Arabia, Cardi B anaendelea kuonyesha kuwa ushawishi wake hauishii kwenye muziki pekee, bali pia unaendelea kukua katika mitindo, utamaduni na burudani ya kimataifa.

Stori na Nasra Kassim | GPL – TUDACO

Exclusive: Saleh Ally Afichua Siri ya Safari Yake Katika Uandishi wa Habari za Michezo – Video

Global Publishers
August 29, 2026
1,128 views
0 Comments

Mwandishi mahiri wa habari za michezo nchini Tanzania, Saleh Ally (@salehjembefacts), amefanya mahojiano maalum (exclusive interview) na Global TV, ambapo amefunguka kwa kina kuhusu safari yake ya uandishi wa habari za michezo na mambo mbalimbali ambayo wengi hawakuyajua kuhusu maisha yake ya kikazi.

Katika mahojiano hayo, Saleh Ally amezungumzia kwa undani safari yake katika taaluma ya uandishi wa habari, changamoto alizokutana nazo pamoja na matukio yaliyokuwa na mchango mkubwa katika kujenga jina lake kwenye tasnia ya habari za michezo nchini.

Miongoni mwa mambo aliyoyafichua ni kuhusu mahojiano yake makubwa ya kwanza aliyowahi kufanya na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea F.C. na Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba.

Saleh Ally amesema mahojiano hayo na Drogba yalikuwa miongoni mwa matukio muhimu yaliyomfungulia milango katika safari yake ya kutimiza ndoto yake ya kuwa mwandishi mahiri wa habari za michezo.

Kwa mujibu wa Saleh Ally, fursa hiyo haikuwa tu mahojiano ya kawaida na nyota mkubwa wa soka, bali ilikuwa hatua muhimu iliyompa msukumo, kujiamini na kumfungulia njia ya mafanikio katika taaluma aliyokuwa akiipenda.

Katika mahojiano hayo na Global TV, Saleh Ally pia amegusia mambo mengine mengi kuhusu maisha yake, safari yake ya kikazi, namna alivyokutana na changamoto mbalimbali na matukio yaliyomsaidia kufika alipo leo.

Nafasi za Kazi kwa Wanawake – Wahudumu wa Maduka Mlimani City na Posta

Global Publishers
August 29, 2026
1,392 views
0 Comments

Nafasi za kazi zimetangazwa kwa wanawake pekee kwa ajili ya kufanya kazi kama Wahudumu wa Maduka katika maeneo ya Mlimani City na Posta, Dar es Salaam.

Mshahara: TSh 450,000 kwa mwezi.

Sifa za mwombaji:

  • Awe mwanamke.
  • Awe mchapakazi, mwaminifu na mwenye nidhamu.
  • Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wateja.
  • Uzoefu wa kazi ni faida.

Jinsi ya kuomba

Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia WhatsApp: 0747065803.

Kumbuka: Nafasi hizi ni kwa wanawake pekee na nafasi ni chache. Waombaji wanashauriwa kutuma maombi mapema.

‘Starrgirl’ Yafanya Makubwa Billboard, Ayra Starr Atoboa Top 4

Mwimbaji wa Nigeria, Ayra Starr.

Mwimbaji wa Nigeria, Ayra Starr, ameendelea kuonyesha nguvu ya muziki wa Afrika katika soko la kimataifa baada ya album yake mpya “Starrgirl” kuingia katika nafasi ya nne kwenye Billboard World Albums Chart.

Mafanikio hayo yanaifanya “Starrgirl” kuwa miongoni mwa miradi iliyofanya vizuri kwenye chati hiyo, huku Ayra Starr akiendelea kujenga jina lake katika soko la muziki duniani.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ayra Starr kuingia kwenye Billboard World Albums Chart kupitia album yake kama msanii wa solo, hatua inayochukuliwa kuwa moja ya mafanikio makubwa katika safari yake ya muziki pamoja na kuongeza heshima kwa muziki wa Nigeria.

Album hiyo ilitolewa rasmi Agosti 14, 2026, kupitia Mavin Records na Republic Records, ikiwa ni album yake ya tatu ya studio.

“Starrgirl” inafuatia album zake mbili zilizotangulia, “19 & Dangerous” iliyotoka mwaka 2021 na “The Year I Turned 21” iliyotolewa mwaka 2024.

Album hiyo ina jumla ya nyimbo 16, huku Ayra Starr akiwashirikisha baadhi ya majina makubwa kutoka Nigeria na kimataifa, akiwemo Wizkid, Rema, ZAYN, Leon Thomas, kwn, Theodora na Danny Ocean.

Miongoni mwa nyimbo zinazopatikana kwenye album hiyo ni “Gimme Dat” akiwa na Wizkid, “Who’s Dat Girl” akiwa na Rema na “Heaven Baby” akiwa na ZAYN.

“Starrgirl” Yawa Mbele ya Album ya Tyla

Katika Billboard World Albums Chart, “Starrgirl” imeingia katika nafasi ya nne, ikiwa nyuma ya miradi mitatu ya K-pop.

Nafasi ya tano imechukuliwa na album “APOP” ya msanii wa Afrika Kusini, Tyla, hivyo Ayra Starr ameweka “Starrgirl” mbele ya album hiyo katika chati.

Mafanikio hayo yamekuja ndani ya muda mfupi tangu album hiyo itoke, jambo linaloendelea kuongeza uzito wa Ayra Starr katika muziki wa Afrobeats na soko la muziki la kimataifa.

Kwa kuingia katika nafasi ya nne kwenye Billboard, Ayra Starr anaendelea kuthibitisha kuwa wasanii wa Afrika wana uwezo wa kushindana katika majukwaa makubwa ya muziki duniani na kuvuka mipaka ya bara hilo.

Stori na Razaku Ramadhan | GPL – TUDACO

Baada ya Kimya, Mwijaku Amtaka Maua Sama Aachie Muziki Mpya

Mjadala kuhusu kurejea kwa msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama, katika muziki umeibuka upya baada ya mwanahabari na mchambuzi wa burudani Mwijaku kumtaka msanii huyo kuanza kutoa kazi mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo, Agosti 27, 2026, Mwijaku ametoa ujumbe mfupi lakini wenye uzito kwa Maua Sama, akisisitiza kuwa mashabiki wake bado wanahitaji kusikia muziki mpya kutoka kwake.

“Tunataka nyimbo mpya,” aliandika Mwijaku.

Kauli hiyo imeibua hisia mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakionyesha hamu ya kumuona Maua Sama akirejea studio na kuendelea na safari yake ya muziki.

Maua Sama ni miongoni mwa wasanii wa kike waliowahi kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva na Afro-Pop nchini Tanzania.

Alijenga jina kupitia nyimbo mbalimbali zilizopokelewa na mashabiki, ikiwemo “Iokote”, ambayo ilichangia kuongeza umaarufu wake katika tasnia ya muziki.

Kwa kipindi cha hivi karibuni, mashabiki wamekuwa wakisubiri kusikia kazi mpya kutoka kwa msanii huyo, huku maisha yake binafsi yakionekana kuchukua sehemu kubwa ya muda wake.

Ujumbe wa Mwijaku umeongeza matarajio kwa mashabiki wanaotamani kumuona Maua Sama akirudi kwenye muziki.

Kwa kuwa tayari ana historia na msingi wa mashabiki katika tasnia hiyo, kurejea kwake kwa kazi mpya kunaweza kuongeza ushindani katika muziki wa kike na kutoa hamasa mpya kwa mashabiki wa Bongo Fleva.

Kwa sasa, bado haijafahamika iwapo Maua Sama amepanga kutoa kazi mpya, lakini ujumbe wa Mwijaku umeweka wazi jambo moja mashabiki bado wanaisubiri sauti yake.

Stori na Nasra Kassim | GPL -TUDACO

Jux Atoa Tamko Kuhusu Madai ya Mtoto “Sheria Kuchukua Mkondo”

Msanii Juma Jux ametoa tamko kwa umma akikanusha madai yanayosambaa yakimuhusisha kuwa baba wa mtoto wa mtu fulani, akisema taarifa hizo hazina ukweli na sasa suala hilo limefikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kupitia tamko hilo, Jux amesema amekuwa akifuatilia suala hilo kwa utulivu bila kulipa uzito, kwa kuwa awali aliona halina msingi wala halistahili kupewa nafasi, lakini ameamua kulizungumzia baada ya madai hayo kuendelea kuhusisha jina lake, familia yake, biashara zake na taswira aliyoijenga kwa miaka mingi kwa jasho na kazi kubwa.

Jux amesema suala hilo liliwahi kujitokeza hapo nyuma, ambapo kwa kutaka kujiridhisha kuhusu chanzo cha madai hayo, alichukua hatua ya kumtafuta mhusika mwenyewe ili kufahamu ni kwanini alikuwa akisema alichokuwa amekisema hapo awali.

Kwa mujibu wa Jux, mhusika huyo alithibitisha kwa maneno na kwa sauti yake kuwa hakuwahi kukutana naye kimwili wala kuwa na mahusiano ya kimapenzi naye.

Aidha, Jux amesema mhusika huyo alimuomba asilipe uzito suala hilo, akieleza kuwa madai hayo yalitokana na maoni ya baadhi ya mashabiki waliokuwa wakimfananisha mtoto huyo na Jux, jambo lililopelekea baadhi yao kuanza kumhusisha kuwa baba wa mtoto.

Hata hivyo, Jux amesema madai hayo yameibuka tena na sasa yamechukua mwelekeo tofauti, hali iliyomfanya kuchukua hatua za kisheria.

Amesema suala hilo kwa sasa lipo mikononi mwa vyombo vya sheria, huku akieleza kuwa hatua zaidi zitachukuliwa dhidi ya mhusika.

Jux pia ametoa rai kwa vyombo vya habari na watu mbalimbali kuepuka kusambaza taarifa za kupotosha bila kuwa na uhakika wa ukweli wake, akisisitiza kuwa taarifa zisizo na ukweli zinaweza kuathiri jina, familia na biashara ya mtu.

Katika tamko lake, Jux amesema amejenga jina lake, brand na biashara zake kwa miaka mingi kupitia kazi, nidhamu na kujituma, hivyo mtu yeyote anayechagua kuhusisha jina lake, familia yake au biashara zake na madai yasiyo ya kweli, atalazimika kuwajibika kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Jux amesema amechagua kubaki katika utulivu na kusimamia ukweli, huku akiacha hatua zaidi zichukuliwe kupitia njia sahihi za kisheria.

“Kwa upande wangu, nimechagua utulivu, ukweli na hatua sahihi za kisheria,” Jux amesema katika tamko lake.

STORI NA Na DIDAS DIDAS | GPL -TUDACO

Fahamu Maajabu ya Kula Samaki na Faida Zake kwa Mwili

Samaki ni miongoni mwa vyakula vinavyopendwa na watu wengi kutokana na ladha yake, lakini zaidi ya kuwa chakula kitamu, samaki wana virutubisho muhimu vinavyoweza kuchangia afya na ustawi wa mwili.

Aina mbalimbali za samaki zina protini, vitamini, madini na mafuta yenye manufaa kama Omega-3. Kula samaki kama sehemu ya lishe yenye uwiano kunaweza kuwa na faida kadhaa kwa mwili.

1. Husaidia afya ya moyo

Samaki wenye mafuta, kama dagaa, sardini na salmon, wana Omega-3 ambayo inahusishwa na afya nzuri ya moyo na mishipa ya damu.

Kula samaki mara kwa mara kama sehemu ya lishe bora kunaweza kusaidia kupata mafuta yenye manufaa badala ya kutegemea zaidi vyakula vyenye mafuta yasiyofaa.

2. Huchangia afya ya ubongo

Omega-3 ni miongoni mwa virutubisho muhimu vinavyohitajika kwa utendaji wa kawaida wa ubongo.

Ndiyo maana samaki wamekuwa wakihusishwa na lishe inayosaidia afya ya ubongo, huku samaki wenye mafuta wakiwa chanzo kizuri cha aina hii ya mafuta.

3. Ni chanzo kizuri cha protini

Mwili unahitaji protini kwa ajili ya kujenga na kurekebisha misuli pamoja na tishu nyingine.

Samaki wengi wana protini yenye ubora mzuri, jambo linalowafanya kuwa sehemu muhimu ya mlo kwa watu wanaotaka kupata chanzo kizuri cha protini.

4. Husaidia afya ya macho

Samaki wenye mafuta wana Omega-3 na virutubisho vingine vinavyohusishwa na afya ya macho.

Kuwa na lishe yenye samaki, mboga, matunda na vyakula vingine vyenye virutubisho mbalimbali kunaweza kusaidia kudumisha afya ya macho.

5. Hutoa vitamini na madini muhimu

Samaki wanaweza kuwa chanzo cha virutubisho kama vitamini B12, vitamini D, selenium, iodine na zinc, ingawa kiwango hutofautiana kulingana na aina ya samaki.

Vitamini B12, kwa mfano, ni muhimu kwa utendaji wa kawaida wa mfumo wa neva na utengenezaji wa chembe nyekundu za damu.

6. Dagaa wanaweza kusaidia kuongeza calcium

Dagaa wadogo wanaoliwa pamoja na mifupa yao wanaweza kuwa chanzo kizuri cha calcium.

Calcium ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno, hivyo dagaa wanaweza kuwa sehemu nzuri ya lishe yenye virutubisho mbalimbali.

7. Ni chakula kinachoweza kuwa na mafuta machache

Baadhi ya samaki wana kiasi kidogo cha mafuta na wanaweza kuwa chaguo zuri kwa mtu anayezingatia mlo wenye uwiano.

Hata hivyo, namna samaki wanavyopikwa ina umuhimu. Samaki wa kuchemsha, kuoka au kuchoma wanaweza kuwa na mafuta machache zaidi kuliko samaki waliokaangwa kwa mafuta mengi.

Samaki wale mara ngapi?

Kwa ujumla, wataalamu wa lishe wanashauri samaki kuwa sehemu ya mlo wa mara kwa mara. Kubadilisha aina za samaki kunaweza kusaidia kupata mchanganyiko mpana wa virutubisho.

Pia ni muhimu kuzingatia ukubwa wa samaki. Baadhi ya samaki wakubwa wanaweza kukusanya kiwango kikubwa cha zebaki, hivyo matumizi ya aina mbalimbali za samaki yanaweza kusaidia kupunguza ulaji wa zebaki kwa kiwango kikubwa.

Jinsi ya kupata faida zaidi

Ili kupata manufaa zaidi kutokana na samaki, ni vizuri kuzingatia namna wanavyotayarishwa. Kuchemsha, kuoka au kuchoma kunaweza kuwa chaguo bora kuliko kukaanga kwa mafuta mengi.

Samaki pia anaweza kuunganishwa na mboga, nafaka zisizokobolewa na vyakula vingine vyenye virutubisho ili kutengeneza mlo wenye uwiano.

Hitimisho

Kula samaki kunaweza kuwa na nafasi muhimu katika lishe yenye afya. Kutokana na kuwa chanzo cha protini, Omega-3, vitamini na madini mbalimbali, samaki wanaweza kusaidia afya ya moyo, ubongo, misuli, macho na mifupa.

Hata hivyo, hakuna chakula kimoja kinachoweza kutoa kila kirutubisho kinachohitajika na mwili. Kwa hiyo, siri ni kuwa na mlo wenye mchanganyiko wa vyakula mbalimbali, kula samaki kwa kiasi kinachofaa na kuchagua njia bora za kuwatayarisha.

Kitawaka EPL Wikiendi Hii, Macho Yatakuwa Liverpool, United, Arsenal

Ligi Kuu ya England, Premier League, inaendelea wikiendi hii kwa michezo mbalimbali huku timu kubwa zikitarajiwa kushuka dimbani kuwania pointi muhimu katika mbio za mapema za msimu wa 2026/27.

Miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu ni Liverpool dhidi ya Nottingham Forest, huku Liverpool ikilenga kuendeleza kasi nzuri na kuhakikisha inapata matokeo yatakayoipa nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Nayo Tottenham Hotspur itakuwa mwenyeji wa Newcastle United katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Timu hizo zinahitaji pointi tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Macho pia yataelekezwa kwenye mchezo wa Brighton dhidi ya Chelsea, ambapo Chelsea itakuwa ikitafuta ushindi muhimu dhidi ya Brighton. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na mvuto kutokana na ushindani wa timu hizo katika soka la England.

Katika mchezo mwingine mkubwa, Aston Villa itakutana na Arsenal, huku Arsenal ikitarajiwa kuwa na kazi ya kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika uwanja wa Villa.

Kwa upande wa Manchester United, timu hiyo itakuwa ugenini dhidi ya Ipswich Town katika mchezo utakaokuwa muhimu kwa kikosi hicho, hasa baada ya kuanza msimu kwa matokeo yasiyoridhisha.

Wakati huo huo, michezo mingine ya wikiendi itawakutanisha Bournemouth na Everton, Sunderland na Fulham, pamoja na Leeds United dhidi ya Brentford.

Kwa ujumla, wikiendi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikisaka pointi tatu katika hatua za mwanzo za msimu wa Premier League.

Wiki hii ndani ya DStv ni special sana! Usikose kutazama episode mpya ya kipindi cha A List, mechi za kukatana na shoka za ligi ya England, bila kusahau Jumapili kuanzia saa 4:00 tunaanza kuitazama series mpya ya Spinners ikiwa na lugha ya Kiswahili.

Mechi za EPL wikiendi hii — 29–31 Agosti 2026

Ijumaa, Agosti 28

  • Crystal Palace vs Manchester City — saa 4:00 usiku (Tanzania)

Jumamosi, Agosti 29

  • Liverpool vs Nottingham Forest — saa 2:30 jioni
  • Bournemouth vs Everton — saa 5:00 jioni
  • Coventry City vs Hull City — saa 5:00 jioni
  • Tottenham Hotspur vs Newcastle United — saa 7:30 usiku

Jumapili, Agosti 30

  • Sunderland vs Fulham
  • Brighton vs Chelsea
  • Leeds United vs Brentford
  • Aston Villa vs Arsenal

Jumatatu, Agosti 31

  • Ipswich Town vs Manchester United

Ratiba hii ni ya wikiendi ya pili ya Premier League 2026/27.