Rais Samia Ateua na Kuhamisha Wakuu Wa Mikoa, Makatibu Tawala
Global Publishers
August 27, 2026
54 views
0 Comments

Dar es Salaam, Agosti 27, 2026 — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu, uteuzi na uhamisho huo umefanyika kama ifuatavyo:
UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA
- CP. Salum Rashid Hamduni, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
- Alexander Pastory Mnyeti ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.
- Stanslaus Haroon Nyongo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
- Jumanne Abdallah Sagini ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
UHAMISHO WA WAKUU WA MIKOA
- Martine Reuben Shigela amehamishwa kutoka Mkoa wa Geita kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
- Said Mohamed Mtanda amehamishwa kutoka Mkoa wa Mwanza kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, akichukua nafasi ya Anamringu Macha ambaye amestaafu.
- Abubakar Mussa Kunenge amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, akichukua nafasi ya Jabiri Omari Makame, ambaye atapangiwa majukumu mengine.
- Beno Moris Malisa amehamishwa kutoka Mkoa wa Mbeya kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Anachukua nafasi ya Paul Matiko Chacha, ambaye aliteuliwa kuwa Katibu wa NEC – Idara ya Oganaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
- Adam Kighoma Malima amehamishwa kutoka Mkoa wa Morogoro kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, akichukua nafasi ya Zainab Telack, ambaye amestaafu.
- Queen Cuthbert Sendiga amehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
UTEUZI NA UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA
Uteuzi
Richard Marcellino Kayombo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.
Uhamisho
- Bw. Balandya Mayuganya Elikana amehamishwa kutoka Mkoa wa Mwanza kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya.
- Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga amehamishwa kutoka Mkoa wa Singida kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
- Pili Hassan Mnyema amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
- Rodricks Lazaro Mpogolo amehamishwa kutoka Mkoa wa Mbeya kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa upashaji wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
Uteuzi na uhamisho huo umetangazwa na Ikulu, Dar es Salaam, Agosti 27, 2026.