Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Sample Page
  • Home
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

Binti auawa kwa madai ya kupigwa na baba yake mdogo, kisa sherehe ya tohara

By admin
August 19, 2026 2 Min Read
Comments Off on Binti auawa kwa madai ya kupigwa na baba yake mdogo, kisa sherehe ya tohara

Rorya. Mkazi wa Kijiji cha Isango, Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Jackline Mteresa (18), amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa na baba yake mdogo kwa tuhuma za kuchelewa kurejea nyumbani baada ya kwenda kwenye sherehe ya tohara.

Katika tukio hilo, Rhobi Werema (16), ambaye ni mtoto wa mtuhumiwa, amelazwa katika Kituo cha Afya Kinesi kwa matibabu baada ya kudaiwa kujeruhiwa kwa kipigo kutoka kwa baba yake mzazi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Mark Njera, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jeshi la Polisi limeanza msako wa kumtafuta mtuhumiwa.



Akizungumza leo Jumatano, Agosti 19, 2026, Njera amesema tukio hilo lilitokea Agosti 17, saa 10 jioni katika Kijiji cha Isango, baada ya Jackline kwenda kwenye sherehe ya tohara iliyofanyika kijijini hapo siku moja kabla.

“Ni kweli kuna tukio hilo. Binti huyo alifariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa kwa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili na baba yake mdogo. Jina la mtuhumiwa linahifadhiwa kwa sababu za upelelezi. Jeshi la Polisi limeanza msako baada ya kutoroka,” amesema.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, ambaye hakutaka jina lake litajwe, Jackline alienda kwenye sherehe hiyo akiwa ameongozana na Rhobi na walipokuwa wakirejea nyumbani, mtuhumiwa aliwafuata na kuanza kuwapiga.

Amesema kipigo hicho kilisababisha Jackline kuanguka na kujigonga kwenye jiwe na kupoteza fahamu.

“Walimbeba Jack na kumpeleka nyumbani, kisha kumpatia huduma ya kwanza. Alipozinduka, akaendelea kumpiga. Ikafika hatua mtoto akaanza kuomba maji ya kunywa, lakini hakupata msaada wowote. Rhobi alifanikiwa kukimbia,” amesema.

Ndugu huyo amesema baadaye Jackline alikata kauli na majirani walipofika walimchukua na kumpeleka Kituo cha Afya Kinesi, lakini walipofika alikuwa tayari amefariki dunia.

Amesema baada ya daktari kuthibitisha kifo hicho, mtuhumiwa alitoroka na hadi jana hakuwa amekamatwa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika kituo hicho cha afya, huku taratibu za mazishi zikisubiri kuwasili kwa baba yake.

Amesema Jackline alikuwa akiishi na baba yake huko Kahama mkoani Shinyanga baada ya wazazi wake kutengana na wakati mwingine alikuwa akiishi kwa bibi yake.

Kwa mujibu wa ndugu huyo, Jackline alikwenda kwa bibi yake mzaa baba kwa ajili ya kumsalimia na alikuwa amefika eneo hilo takriban wiki moja kabla ya tukio.

Ndugu huyo ameliomba Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa ili sheria ichukue mkondo wake, akidai kuwa kuna uwezekano wa kuwa amefichwa na ndugu zake.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Isango, Kichere Magesa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio.

“Ni kweli kuna hilo tukio hapa kijijini kwetu na anayedaiwa kufanya tukio hilo ametoroka. Kuna uwezekano mazishi yakafanyika kesho,” amesema.

Kichere amesema baba wa marehemu, anayeishi Kahama, alipewa taarifa kuhusu tukio hilo lakini hadi jana hakuwa amefika kijijini hapo.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

PROF. MKUMBO: HALMASHAURI ZIBUNI SHUGHULI MPYA ZA KIUCHUMI, SI TOZO MPYA.

Next

SHILINGI BILIONI 356 ZATUMIKA KUTEKELEZA MIRADI MOROGORO

Recent Posts

  • Mambo wachumba wanayosahau kabla ya ndoa, madaktari waonya
  • Kesi ya ugaidi mhadhiri UDOM, vigogo CWT zatupwa wiki ijayo
  • DC HAI AENDELEA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI, ATATUA MIGOGORO YA ARDHI
  • Wamiliki miundombinu muhimu ya Tehama watakiwa kuisajili
  • SHILINGI BILIONI 356 ZATUMIKA KUTEKELEZA MIRADI MOROGORO

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme