Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

BIBI ANAYEISHI NA WATOTO WENYE CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI AFUTWA MACHOZI NA DKT.TULIA

By admin
August 28, 2026 3 Min Read
Comments Off on BIBI ANAYEISHI NA WATOTO WENYE CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI AFUTWA MACHOZI NA DKT.TULIA

 

Na Matukio Daima Media, Mbeya

 BIBI Grace Deya (70), mkazi wa Mtaa wa Tembela, Kata ya Tembela katika Jimbo la Uyole mkoani Mbeya amefutwa machozi baada ya Taasisi ya Tulia Trust kuamua kumjengea nyumba kutokana na hali ngumu ya maisha anayokabiliana nayo pamoja na watoto wake watatu wenye changamoto za afya ya akili.

Bibi huyo amekuwa akiishi katika nyumba chakavu na kutegemea msaada kutoka kwa majirani, huku akitakiwa kuwahudumia watoto wake ambao ni watu wazima na wenye changamoto za afya ya akili.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 27,2026 kuhusu mpango wa ujenzi wa nyumba hiyo, Ofisa Uhusiano na Mahusiano wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo, amesema uamuzi wa kumsaidia Bibi Deya umefikiwa baada ya uongozi wa Mtaa na Kata ya Tembela kufanya tathmini na kubaini kuwa familia hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa.

Mwakanolo amesema ujenzi huo ni sehemu ya shughuli za Taasisi ya Tulia Trust katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, huku wakilenga kuhakikisha nyumba hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa familia hiyo ifikapo Septemba 25, 2026.

«“Sisi Taasisi ya Tulia Trust kwa kushirikiana na uongozi wa kata hii tumeangalia changamoto alizonazo huyu bibi na kubaini kuwa ni kubwa zaidi kuliko familia nyingine. Kwa kuwa tunaadhimisha miaka 10 ya Tulia Trust, tunaamini nyumba hii itajengwa kwa haraka zaidi na tutaikabidhi Septemba 25 mwaka huu, siku moja kabla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 10 ya Tulia Trust,” amesema Mwakanolo.»

Amesema hadi sasa Taasisi hiyo imejenga jumla ya nyumba 26 katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya, ambapo nyumba mbili zimejengwa mkoani Morogoro na nyingine mkoani Ruvuma.

Akizungumza kupitia mkalimani, Diwani wa Kata ya Tembela, kutokana na kutokujua kuzungumza Kiswahili, Bibi Deya amesema amekuwa akikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata chakula, mavazi, malazi na mahitaji mengine muhimu ya kila siku.

«“Nawashukuru sana ndugu zangu na hasa Tulia kwa kuniona mimi, kwa sababu maisha yangu yalikuwa magumu. Nilikuwa naishi kwa kuomba. Mume wangu alifariki miaka 10 iliyopita na watoto wangu wana changamoto za afya ya akili,” amesema.»

Kwa upande wake, ndugu wa Bibi Deya, Kimaro Mwayonga, amesema bibi huyo amekuwa akipitia maisha magumu kutokana na kuishi na watoto wake ambao ni watu wazima na wenye changamoto za afya ya akili.

«“Watoto hawa walikuwa wanamfanyia vitu vibaya mama yao na kumtesa. Kwa ujumla, hali ya huyu mama ni ngumu. Amekuwa akiishi kwa kuomba kwa majirani ili maisha yaweze kuendelea yeye na watoto wake ambao ni watu wazima,” amesema.»

Diwani wa Kata ya Tembela, Frank Mwasyoke, amesema mbali na ujenzi wa nyumba hiyo, Dkt. Tulia amekuwa akisaidia wananchi katika huduma za afya, ambapo zaidi ya wananchi 300 wamewezeshwa kupata bima ya afya tangu alipoanza kutoa msaada huo.

«“Mheshimiwa Dkt. Tulia anafanya mambo makubwa katika kata yetu. Tuna kila sababu ya kumshukuru na kumuombea Mungu amwongoze zaidi. Katika historia ya wabunge waliowahi kuongoza Jimbo la Mbeya, tunaona namna ambavyo amegusa maisha ya wananchi wa chini. Leo wana Tembela tunatabasamu kwa msaada huu,” amesema Mwasyoke.

Mwisho.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Tanzania, DR Congo wakubaliana kuwarejesha wakimbizi – HabariLeo

Next

Crystal Palace dhidi ya Manchester City Kutimua Vumbi EPL

Recent Posts

  • ‘NCHIMBI SIO CHAWA’ – WARIOBA
  • TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI YAANZA UKAGUZI KWA WAKUSANYAJI NA WACHAKATAJI WA TAARIFA HIZO NCHINI.
  • HALMASHAURI YA MAFINGA MJINI HATUJAFUKUZA WATUMISHI WA AFYA BADO TUNAUHITAJI -KAIMU MKURUGENZI
  • SERIKALI KUTUMIA SH1.39 TRILIONI KUKARABATI VIFAA TIBA
  • Crystal Palace dhidi ya Manchester City Kutimua Vumbi EPL

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme