Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Sample Page
  • Home
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

MAONESHO YA YST YAIBUA HAMASA YA SAYANSI KWA WANAFUNZI LINDI

By admin
August 19, 2026 3 Min Read
Comments Off on MAONESHO YA YST YAIBUA HAMASA YA SAYANSI KWA WANAFUNZI LINDI

Na Hadija omary 

Maonesho ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania YST yameelezwa kuwa ni chachu na hamasa kwa Mkoa wa Lindi katika kuongeza ushiriki wa wanafunzi wa shule za sekondari katika masomo ya sayansi na kujifunza kupitia majaribio.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bi. Victoria Mwanziva wakati wa  maonesho ya kazi bunifu za sayansi na teknolojia yaliyofanyika huko  Manispaa ya Lindi.

 Mwanziva amesema maonesho hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuibua vipaji na kuwavutia wanafunzi wengi kupenda na kufaulu masomo ya sayansi.

Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi Tanzania YST, Dkt. Gozibert Kamugisha, amesema huu ni msimu wa tano kwa Mkoa wa Lindi kushiriki maonesho hayo na yamekuwa na manufaa makubwa kwa wanafunzi katika kubuni na kutatua matatizo ya jamii kupitia sayansi.

Amesema YST ni jukwaa ambalo linajitahidi kujenga utamaduni kwa vijana kwa kufanya utafiti na kugundua vitu vipya kiasi kwamba Hata wanavyoendelea kukua na kuendelea na masomo Yao utafiti uwe ni swala la kiutamaduni na lisiwe swala la kuelekezwa.” alieleza Kamugisha

Ameongeza kuwa lengo la kuyafanyia hayo yote ni kutengeneza kizazi ambacho kinaweza kuchukua jukumu la moja kwa moja kumaliza matatizo yanayowakabili Watu kuliko kusubiri Serikali ama wafadhiri kwa ajili ya kutatua matatizo hayo.

Aidha Mshauri wa Masuala ya Kijamii kutoka Kampuni ya Shell ambao ni wadhamini wa maonesho hayo, Bi. Msomis  Mbena, amesema kupitia program hiyo wanafunzi wamewezeshwa kufanya bunifu mbalimbali zitakazosaidia kutatua changamoto za kila siku. 

“Program hii ya YST inaendana na mikakati wetu wa kimataifa wa kundeleza elimu ya Sem huku ikichangia maendeleo ya ujuzi kwa kuwasaidia wanafunzi kukuza uwezo wa kufanya utafiti, ugunduzi pamoja na kutafuta  changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii” alisema Mbena 

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Lindi  Mwalimu Rehema Nahale ametumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa YST kwa msaada wao wa kuwasaidia wanafunzi kufanya uvumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayotokea katika jamii .

” Hakika nafasi hii ni kubwa Sana kwao na wataichukua elimu hii sio tu kwa kujifunza kwa ubinafsi wao bali watasaidia matatizo ya jamii kwa ujumla lakini hii itakuwa faida kwao kwa elimu ya kivitindo itakuwa imebaki vichwani mwao ” alisema Nahale

Katika maonesho hayo shule tatu  zilizoshinda zimepata nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa Lindi katika mashindano ya kitaifa yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Ebola yazidi kutikisa DR Congo, vifo vyafikia 2,378

Next

SERIKALI YATOA MIEZI SITA KUSAJILI MIUNDOMBINU MUHIMU YA TEHAMA

Recent Posts

  • Kilomita sita kufuata matibabu zawasukuma Kola kujenga zahanati 
  • FIFA IMEJIHARIBIA YENYEWE KWA MPANGO WA KOMBE LA DUNIA – MKUU WA LIGI KUU YA UINGEREZA
  • SERIKALI YATOA MIEZI SITA KUSAJILI MIUNDOMBINU MUHIMU YA TEHAMA
  • MAONESHO YA YST YAIBUA HAMASA YA SAYANSI KWA WANAFUNZI LINDI
  • Ebola yazidi kutikisa DR Congo, vifo vyafikia 2,378

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme